Watu wengine 603 wamegunduliwa kuwa na virusi vya corona nchini huku idadi jumla ya visa vya maambukizi ikifikia 13,353.
Akitangaza matokeo hayo Jumapili, Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe pia alifichua kuwa watu wengine 682 walipona virusi hivyo na kupelekea idadi ya waliopata nafuu kuongezeka kutoka 4,440 hadi 5,122.
Hata hivyo, waziri huyo alithibitisha kuwa wagonjwa wengine tisa waliaga dunia na kuongezea katika idadi jumla ya 225 iliyorekodiwa Jumamosi, Julai 18, hadi 234.
“Takwimu ya hii leo ya hali ya COVID-19 nchini inaonyesha bado visa vya maambukizi vinaendelea kuongezeka. Tunaendelea kuwaomba watu wetu wachukue tahadhari na mikakati ya kujilinda kwa makini,” alisema Kagwe.
Kufikia Jumapili, Julai 19, visa vya COVID-19 viliongezeka maradufu hadi 14,458,857 ulimwenguni ikiwemo idadi ya 8,643,379 ya waliopona na vifo 605,694.