Connect with us

General News

Mzozo wa Ukraine kutatiza Wakenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mzozo wa Ukraine kutatiza Wakenya – Taifa Leo

Mzozo wa Ukraine kutatiza Wakenya

NA PETER NGARE

MZOZO kati ya Urusi na Ukraine utasababisha ongezeko la bei za bidhaa muhimu kwa Wakenya hasa zinazotengenezwa kwa ngano.

Licha ya Kenya kuwa umbali wa takriban kilomita 9,000 kutoka Urusi, uwezekano wa taifa hilo kuanzisha vita dhidi ya jirani yake Ukraine pia utaathiri uagizaji wa chuma pamoja na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta.

Kiasi kikubwa cha ngano inayotumika hapa Kenya huagizwa kutoka Ukraine na Urusi, na kuzuka kwa vita baina ya mataifa hayo kutasababisha uhaba na hivyo kuongeza bei za bidhaa kama vile mkate na unga wa ngano.

Wakulima wa majani chai pia wataumia kwani Urusi hununua kiasi kikubwa cha bidhaa hiyo kutoka Kenya, ikiwa ndiyo mteja nambari nne duniani wa majani chai ya Kenya.

Amerika imetishia kuwekea Urusi vikwazo vikali vya kiuchumi iwapo itavamia Ukraine, ikiwemo kuzimwa kutumia Dola katika biashara, hali ambayo itaathiri uuzaji wa majani chai ya Kenya nchini humo pamoja na uagizaji wa ngano na chuma kutoka taifa hilo.

Bei ya mafuta pia inatarajiwa kupanda kutoka Sh9,500 kwa pipa hadi Sh15,000, hali ambayo itaongeza gharama ya mafuta nchini na pia ya bidhaa zingine.

Rais Vladimir Putin wa Urusi mnamo Jumatatu alitangaza kutambua mikoa miwili ndani ya Ukraine kuwa huru, hatua iliyolaumiwa na mataifa mengi Jumanne ikiwemo Kenya.

Urusi imepeleka wanajeshi kwenye mpaka wake na Ukraine ambayo ni mshirika wa mataifa ya Uropa na Amerika.

Putin alisema Jumanne amekasirishwa na NATO kupeleka zana za kivita karibu na Urusi, pamoja na kupanga kujiunga na Muungano wa Uropa (EU).

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending