Connect with us

General News

Uwanja wa Wembley kuwa mwenyeji wa gozi la Finalissima kati ya Italia na Argentina mnamo Juni 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uwanja wa Wembley kuwa mwenyeji wa gozi la Finalissima kati ya Italia na Argentina mnamo Juni 2022 – Taifa Leo

Uwanja wa Wembley kuwa mwenyeji wa gozi la Finalissima kati ya Italia na Argentina mnamo Juni 2022

Na MASHIRIKA

UWANJA wa Wembley nchini Uingereza utakuwa mwenyeji wa kipute kilichofufuliwa cha ‘Finalissima’ kitakachokutanisha mabingwa wa bara Ulaya, Italia, na wafalme wa Copa America, Argentina mnamo Juni 1, 2022.

Vinara wa Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa) na wale wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (Conmebol) waliafikiana mnamo 2021 kuhusu jinsi makala matatu yajayo ya Finalissima yatafanyika.

Mnamo Disemba 2021, ilithibitishwa kwamba jiji la London lingekuwa mwenyeji wa makala ya kwanza na sasa ni rasmi kwamba kivumbi hicho kitafanyika ugani Wembley.

Itakuwa mara ya kwanza tangu 1993 kwa mashindano ya Finalissima kufanyika. Diego Maradona alichezea Argentina walioshinda taji la Copa America mnamo 1991 katika gozi hilo la Finalissima na akaongoza timu yake ya taifa kukomoa Denmark waliotawazwa wafalme wa Euro 1992.

Mechi ya Finalissima mwaka huu itashuhudia Italia wakirejea katika uwanja uliowapa jukwaa la kukomoa Uingereza na kutwaa taji la Euro. Argentina walitawazwa mabingwa wa Copa America mnamo Juni 2021 baada ya kuzamisha wenyeji Brazil jijini Rio de Janeiro.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO