Connect with us

General News

Tutamkomesha Putin! – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Tutamkomesha Putin! – Taifa Leo

Biden: Tutamkomesha Putin!

NA MASHIRIKA

WARSAW, POLAND

RAIS Joe Biden wa Amerika, Jumamosi alimtaja Rais Vladimir Putin wa Urusi kuwa “kiongozi mkatili ambaye hawezi kuruhusiwa kuendelea kuwa mamlakani.”

Kwenye hotuba kali aliyotoa jijini Warsaw, Poland, baada ya kukutana na mawaziri wa ngazi za juu wa Ukraine, Rais Biden alisema kuwa “watafanya kila wawezalo kukomesha ukatili wa Putin.”

“Usifikirie (Putin) kuhusu uwezekano wa kuingia katika nchi moja ya himaya za nchi washirika wa Shirika la Kujihami (NATO),” akasema Biden.

Kwenye taarifa baada ya kauli hiyo, Ikulu ya White House ilisema kuwa lengo la Amerika si kubadilisha uongozi nchini Urusi, bali inasikitishwa sana na ukatili unaoendelezwa na Putin dhidi ya watu wasio na hatia nchini Ukraine.

Lakini mara tu baada ya kauli hiyo, afisa mmoja wa ngazi za juu wa utawala wa Putin alisema kuwa “matamshi ya Biden yanapunguza uwezekano wa mwafaka kupatikana kati ya pande hizo mbili.”

Kwenye hotuba yake, Biden alionekana kuwarai raia wa Urusi kumlaumu Putin kutokana na athari za vikwazo vingi ambavyo taifa hilo limewekewa na mataifa ya Magharibi.

Biden alitoa hakikisho kwa raia wa Ukraine na waathiriwa wengine wa vita hivyo kuwa Amerika “itakuwa nao wakati huu mgumu.”

Kufikia sasa, inakisiwa kuwa karibu watu milioni nne wameachwa bila makao ama kutafuta hifadhi katika mataifa jirani.

“Tutasimama pamoja nanyi,” akasema Biden.

Kiongozi huyo vile vile alitilia shaka ahadi ya Urusi kuwa huenda ikapunguza mashambulio yake dhidi ya taifa hilo.

Hilo lilijiri huku Urusi ikirusha mizinga miwili mashariki mwa Ukraine.

Biden alisema haelewi vile Urusi “imebadilisha malengo yake kighafla.”

Hata hivyo, alieleza kuwa taifa hilo “limeshindwa kabisa kutimiza malengo liliyokuwa nayo awali wakati lilipoanza uvamizi huo.”

Mizinga hiyo ya Urusi ilishambulia kituo cha kusafishia mafuta katika mji wa Lviv, magharibi mwa Ukraine, ulio umbali wa kilomita 45 pekee kutoka mpaka wa Poland.

Gavana wa eneo hilo, Maksym Kozytsky, aliwambia wanahabari kwamba watu watano waliuawa kwenye shambulio hilo.

Rais Putin alituma majeshi yake nchini humo Februari 24, akiapa kuharibu jeshi la taifa hilo na kumpindua Rais Volodymyr Zelensky.

Rais Zelensky ana ushirika wa karibu na mataifa ya nchi za Magharibi.

Licha ya juhudi kubwa za kijeshi ambazo zimekuwa zikiendeshwa na Urusi, zimetajwa kupata mafanikio makubwa.

Biden anakamilisha ziara yake nchini Poland, baada ya kufanya msururu wa mikutano jijini Brussels, Ubelgiji.

Nchini Ubelgiji, alikutana na viongozi wa mataifa ya Magharibi na Waziri wa Mashauri wa Ukraine, Dmytyro Kuleba na mwenzake wa Ulinzi, Oleksii Reznikov.

Jeshi la Urusi limekuwa likilaumiwa kwa kwa kuyalenga maeneo muhimu kama makazi ya watu, hospitali, shule na maeneo walimotafuta hifadhi waathiriwa wa mapigano hayo.

Kwenye kikao na mawaziri hao wawili, imedhihirika pia Amerika imeshusha msimamo wake mkali kuhusu ombi la Ukraine kusaidia na silaha za vita.

Waziri Kuleba alisema kuwa kuna uwezekano baadhi ya ndege za kivita za Amerika zikasafirishwa kutoka Poland hadi Kyiv ili kuyasaidia majeshi ya Ukraine kuikabili vilivyo Urusi.

Awali, makao makuu ya jeshi ya Amerika, Pentangon, yalitaja ombi hilo kuwa “hatari.”

Yalisema kuna hatari hatua hiyo kuongeza mgogoro huo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending