Connect with us

General News

Chipu yataka matayarisho ya mapema Barthes Trophy 2023 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chipu yataka matayarisho ya mapema Barthes Trophy 2023 – Taifa Leo

Chipu yataka matayarisho ya mapema Barthes Trophy 2023

NA GEOFFREY ANENE

BAADA ya kupoteza taji la Kombe la Afrika la raga ya wachezaji 15 kila upande walio chini ya miaka 20, maarufu Barthes Trophy, Kenya inataka matayarisho ya mapema kuelekea makala ya 2023.

Kenya, ambayo iliandaa dimba hilo 2019, 2021 na 2022, pia itakuwa mwenyeji mwaka 2023.

Meneja wa timu Peter Mutai anataka muda zaidi wa kutafuta wachezaji.

“Tunafaa kusaka talanta zaidi chipukizi mwaka mzima,” alisema.

Chipu waliridhika na nishani ya shaba walipozaba Madagascar 49-15 ugani Nyayo, Jumapili.

Vijana wa kocha Curtis Olago walipepeta Uganda 54-20 katika robo-fainali Aprili 9 na kupoteza 16-5 dhidi ya mabingwa wa 2017 na 2018 Namibia katika nusu-fainali Aprili 13 kabla ya kuridhika na nishani ya shaba kwa kuzaba Madagascar 49-15 Aprili 17 ugani Nyayo.

Kenya ilianza maandalizi yake ya Barthes Trophy 2021 mapema mwezi Machi.

Zimbabwe ililemea Namibia 19-14 katika fainali, Tunisia ikanyuka Uganda 24-11 katika mechi ya kuamua nambari tano na sita.

Nayo, Zambia ikaduwaza Ivory Coast 22-8 katika mchuano wa kuamua nafasi mbili za mwisho.Mwenyekiti wa Shirikisho la Raga Kenya (KRU) Oduor Gangla amesema makala ya 2022 yalikuwa ya kufana.

Gangla alishukuru Shirikisho la Raga Afrika (Rugby Africa) kwa kupatia Kenya haki za kuwa mwenyeji na pia kuipiga jeki.

Rais wa Rugby Africa, Khaled Babbou alidhuhuria siku ya mwisho Jumapili.

“Mataifa manane yalishiriki makala haya ambayo ni kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa, lakini tulifaulu kupatia washiriki mashindano mazuri kupitia vifaa vizuri, viwanja, makazi, usafiri, matibabu, viwanja vya mazoezi,” alisema Gangla, akisifu vyombo vya habari kwa kuhakikisha bara lote la Afrika limepata burudani hilo.

“Tunashukuru Wizara ya Michezo kwa usaidizi mkubwa na kufanikisha mashindano haya na pia Waziri Amina Mohammed na Katibu Joe Okudo kuhudhuria bila ya kusahau wadhamini, kamati andalizi, wenye hiari, wafanyakazi wetu, wanahabari, maafisa wa usalama na asasi za serikali,” alisema.

Mganda Dennis Okello aliibuka mfungaji wa pointi nyingi (42) nao Tanaka Gondomukandapi (Zimbabwe), Geraldo Beukes (Namibia) na Tsiaro Niaina Michel (Madagascar) wakawa wafungaji wa miguso mingi (mitatu kila mmoja).

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending