Connect with us

General News

Timu ya Ruto yaahirisha kampeni Kenya ikiomboleza Kibaki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Timu ya Ruto yaahirisha kampeni Kenya ikiomboleza Kibaki – Taifa Leo

Timu ya Ruto yaahirisha kampeni Kenya ikiomboleza Kibaki

NA CHARLES WASONGA

MUUNGANO wa Kenya Kwanza umeahirisha kampeni zake zote na shughuli nyingine zilizoratibiwa kutoa nafasi kwa maombolezo ya rais mstaafu Mwai Kibaki.

“Kwa heshima ya rais wetu wa zamani mpendwa Mwai Kibaki, ambaye amepumzika, tumesimamisha ziara zetu katika kaunti za eneo la Magharibi mwa Kenya ili tuungane na Wakenya wengine na familia ya marehemu kuomboleza rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya,” Naibu Rais William Ruto akatangaza katika shule ya Upili ya Wavulana ya Musingu, eneobunge la Ikolomani, Kaunti ya Kakamega, Ijumaa, Aprili 22, 2022.

Dkt Ruto alikuwa ameandamana na vinara wengine wa muungano huo Musalia Mudavadi (ANC) na Moses Wetang’ula.

Viongozi hao walifika eneo hilo kuongoza makongamano kujadili maswala ya uchumi eneo la magharibi.

Viongozi hao waliongoza mkutano wa kwanza wa kiuchumi katika kaunti ya Vihiga mnamo Alhamisi.

Mnamo Jumamosi, Aprili 23, 2022, na Jumapili, Aprili 24, 2022, Dkt Ruto na wenzake walikuwa wameratibiwa kuongozi mikutano sawa na hiyo katika kaunti za Bungoma na Busia, mtawalia.

Kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano katika Afisi ya Naibu Rais Emmanuel Tallam, mkutano wa kiuchumi wa Bungoma ungefanyika mjini Webuye na ule wa Busia ungefanyika mjini Busia.