Connect with us

General News

Mbunge ataka wazazi watume maombi ya basari za watoto wao – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mbunge ataka wazazi watume maombi ya basari za watoto wao – Taifa Leo

Mbunge ataka wazazi watume maombi ya basari za watoto wao

NA ALEX KALAMA

MBUNGE wa Kilifi Kaskazini, Bw Owen Baya, ametaka wazazi kuhakikisha wanatuma maombi ya kutafuta basari ili watoto wao waende shuleni.

Afisi ya Hazina ya Kitaifa ya Ustawishaji Maeneobunge katika eneobunge hilo, ilisema imetenga Sh8 milioni za kuwafadhili wanafunzi wa shule za upili.

Bw Baya alisema kati ya fedha hizo, Sh4 milioni zimetengewa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza huku kiwango sawia na hicho kikipewa wanafunzi wanaoendelea.

Akizungumza na wanahabari mjini Kilifi, Bw Baya aliahidi kushirikiana na wazazi eneo hilo ili kuhakikisha kwamba hakuna mtoto atakayesalia nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa karo.

“Wale wazazi wote ambao wanarudisha watoto wao shule na wale ambao wanaingia kwa kidato cha kwanza, nilikuwa nimejua kwamba kutakuja wakati ambapo serikali haijatoa pesa na mimi nikajipanga nikaweka pesa kama Sh8m,” akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending