Connect with us

General News

DCI yamsaka mshukiwa mkuu wa mauaji ya Samuel Mugoh Muvota – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

DCI yamsaka mshukiwa mkuu wa mauaji ya Samuel Mugoh Muvota – Taifa Leo

DCI yamsaka mshukiwa mkuu wa mauaji ya Samuel Mugoh Muvota

NA WANGU KANURI

IDARA ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) inamsaka Dennis Karani Gachoki, mshukiwa mkuu wa mauaji ya Samuel Mugoh Muvota.

Gachoki alikosana na bosi wake Muvota mojawapo ya sababu ikiwa mapato waliyokuwa wagawane kutoka biashara yao haramu ya ‘pishori’ kabla hajampiga risasi mchana eneo la Mirema, Nairobi.

Kulingana na wapelelezi hao, Gachoki amejihami kwa bunduki ambayo alimnyang’anya afisa mmoja wa polisi baada ya sherehe za unywaji pombe kwenye kilabu kimoja Mombasa, Novemba 2020.

Hata hivyo, juhudi za maafisa wa DCI kumkamata zimegonga mwamba huku Gachoki akiweza kuwahonga maafisa punde tu baada ya kukamatwa kwake.

Hata ingawa, DCI inaamini kuwa Gachoki amekwisha vuka boda na kufika nchi jirani.

Marehemu Muvota alikuwa laghai aliyeanzia kwa kubadilisha kadi za kutoa fedha za watu kwenye benki kisha kusambaza pesa zote kwenye akaunti yake.

Baadaye, akaungana na wanawake wenye kupendeza na kuwaajiri watie dawa ya kulevya aina ya ‘tamuu’ kwenye vinywaji vya wanaume vilabuni.

Cha kusikitisha ni kwamba ndoa nyingi zilisambaratika huku wanaume wengine wakilazwa hospitalini na wasioponea kuaga.

Kupitia kazi hiyo, Muvota aliweza kumiliki magari na nyumba nyingi za kifahari huku akiwaoa wanawake 7.

Wapelelezi wa uhalifu wanasema kuwa Muvota alikuwa amekamatwa kwa zaidi ya mara 30 kwa miaka 11 iliyopita huku akishtakiwa kwa ulaghai.

“Muvota amekuwa karibu korti zote kwenye kaunti ya Kiambu na Nairobi. Mara nyingi, angerudisha pesa za walalamikaji wake na kesi kutamatika,” DCI ikaeleza.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending