Connect with us

General News

2 wengine wanaswa na polisi kuhusiana na mauaji kilabuni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

2 wengine wanaswa na polisi kuhusiana na mauaji kilabuni – Taifa Leo

2 wengine wanaswa na polisi kuhusiana na mauaji kilabuni

NA MAUREEN ONGALA

POLISI katika Kaunti ya Kilifi, wamewakamata washukiwa wengine wawili, kuhusiana na mauaji ya mwanamume katika kilabu cha Lexo Lounge wikendi iliyopita.

Wawili hao ni wafanyakazi wa kilabu hicho ambapo Feisal Bushuti Mkongo alifariki.

Ilidaiwa kulikuwa na mvutano baina yake na walinzi wa kilabu kabla afariki.

Mkuu wa polisi wa Kilifi Kaskazini, Bw Jonathan Koech, alithibitisha tukio hilo limewasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ili kutoa mwelekeo.