[ad_1]
DARUBINI YA UKWELI: Uhuru alipotosha kuhusu hatimiliki
ALIPOKUWA akihutubu wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Madaraka mnamo Jumatano, Rais Uhuru Kenyatta alisema mchakato wa kununua na kuuza ardhi unakamilishwa kwa muda saa 48 pekee badala ya miezi sita kama zamani.
Lakini kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Ardhi (www.lands.go.ke) shughuli nzima ya kusajili ardhi hadi kupata hatimiliki huchukua angalau siku 12.
Ukweli wa mambo ni kuwa kuna hatua tano ambapo mbili za mwanzo huchukua siku saba kisha tatu za mwisho huchukua angalau siku tano.
Uamuzi: Rais alipotosha!
[ad_2]
Source link