Connect with us

General News

Gavana ashauri wakazi kutumia vyema mikopo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Gavana ashauri wakazi kutumia vyema mikopo – Taifa Leo

Gavana ashauri wakazi kutumia vyema mikopo

NA STEPHEN ODUOR

GAVANA wa Kaunti ya Tana River, Bw Dhadho Godhana, ametoa wito kwa wakazi watakaopokea mikopo ya kibiashara waitumie vyema na kulipa kwa wakati unaofaa ili kunufaisha wengine.

Akizungumza wakati wa kuzindua hazina ya Inuka inayofadhiliwa na serikali ya kaunti, Bw Godhana alisema imebainika kuna wengi wanaopokea mikopo hiyo ambao huwa hawaitumii vyema huku wengine wakikosa kulipa.

Hazina hiyo ya Sh75 milioni iliyozinduliwa eneo la Bura imenuiwa kusaidia wafanyabiashara wadogo kupata mikopo yenye riba nafuu.

“Nimetekeleza wajibu wangu lakini pia ninawaomba muwajibike kwa pesa mnazoomba. Iwapo tutaona matunda kutokana na mikopo mnayopewa, tutaongeza fedha kwenye hazina hadi Sh300 milioni,” akasema.

Maoni yake yaliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara katika Bunge la Kaunti, Bw Ismail Kodobo, ambaye aliomba wakazi kutumia vyema nafasi waliyopewa.

Hata hivyo, Bw Kodobo alitaka bodi ya hazina hiyo kuhakikisha mikopo inayolewa kwa usawa bila mapendeleo ya kikabila wala kidini.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending