Connect with us

General News

Mchuuzi kutoka Sudan Kusini ashtakiwa wizi wa simu ya Sh80,000 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mchuuzi kutoka Sudan Kusini ashtakiwa wizi wa simu ya Sh80,000 – Taifa Leo

Mchuuzi kutoka Sudan Kusini ashtakiwa wizi wa simu ya Sh80,000

NA RICHARD MUNGUTI

MCHUUZI kutoka Sudan Kusini aliyemezea mate simu ya rununu ya mwanasoka mwenzake ameshtakiwa.

Sunday Johnson Kong alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Peter Mutua.

Kong alikana kwamba alimwibia mwanasoka huyo Joseph Kot simu ya rununu iliyo na thamani ya Sh80,000.

Kong alidaiwa aliiba simu hiyo wakati wa mechi iliyosakatwa katika uga wa NCC ulioko Jamhuri, Nairobi.

Hakimu alifahamishwa Kot alikuwa amempa rafikiye simu hiyo muundo wa iPhone Promax amshikie alipokuwa anaingia uwanjani kusakata dimba.

Kot alimwuliza rafiki huyo ampige picha za video akicheza.

Rafiki huyo hakujua kupiga picha hizo ndipo alimpa Kong.

Baada ya mechi hiyo Kot alienda kuchukua simu yake lakini rafikiye akamweleza ilikuwa na mshtakiwa – Kong.

Kong alikataa kupeana simu hiyo.

Alikamatwa na kushtakiwa kwa wizi wa simu hiyo ya Kot.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000.

Kesi itatengewa siku ya kusikiliwa baada ya wiki mbili.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending