Connect with us

General News

Okutoyi awasili Australia tayari kwa mashindano mawili ya haiba – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Okutoyi awasili Australia tayari kwa mashindano mawili ya haiba – Taifa Leo

Okutoyi awasili Australia tayari kwa mashindano mawili ya haiba

Na GEOFFREY ANENE

MWANATENISI nyota Angella Okutoyi amewasili nchini Australia mnamo Jumatatu adhuhuri tayari kushiriki mashindano ya chipukizi ya J1 Traralgon na Australian Open.

Okutoyi, 17, ambaye aliabiri ndege saa mbili kasoro dakika 20 Jumapili asubuhi, anakamata nafasi ya 60 kwenye viwango bora vya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF) vya chipukizi.

Kabla ya kuabiri ndege, bingwa huyo wa Afrika alieleza Taifa Leo kuwa anatumai kufunga mwaka 2022 ndani ya mduara wa wachezaji 30-bora duniani.

“Nimejiandaa vyema kwa ziara ya Australia. Nafahamu naenda kukutana na wachezaji wazuri. Nitatia bidii nifike angaa robo-fainali,” alisema Okutoyi ambaye atagonga umri wa miaka 18 hapo Januari 29.

Shindano la J1 Traralgon ni Januari 14-19 nayo Australian Open ni Januari 22-29. Droo ya mashindano hayo bado haijafanywa.

Hii haitakuwa mara ya kwanza Okutoyi kushiriki mashindano nje ya Afrika.

Aliwahi kushiriki mashindano ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 14 nchini Amerika, Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani mwaka 2018.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending