Connect with us

General News

Olago ataja wanaraga 37 wa Chipu kujiandaa kwa Kombe la Afrika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Olago ataja wanaraga 37 wa Chipu kujiandaa kwa Kombe la Afrika – Taifa Leo

Olago ataja wanaraga 37 wa Chipu kujiandaa kwa Kombe la Afrika

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA mkuu Curtis Olago amejumuisha wachezaji saba wazoefu katika kikosi cha timu ya taifa ya chipukizi 37 kuanza kujiandaa kwa Kombe la Afrika maarufu kama Barthes Trophy U20 litakalofanyika Nairobi mwezi Aprili.

Wachezaji waliosalia kikosini kutoka kile cha Barthes Trophy 2021 ni saba – John Baraka, Cornelius Mokoro, Tyson Juma Maina, Anderson Oduor, Wilhite Mususi, Joseph Ayiro na Lucky Ishimwe. Baraka alikuwa nahodha mwaka 2021 wakati Chipu ilipepeta Senegal na Madagascar japo kwa jasho ugani Nyayo na kuibuka mshindi.

Kenya itakuwa inatetea taji lake ambalo imeshinda mara mbili mfululizo baada ya ufanisi wa 2019 uwanjani KCB Ruaraka.

Mabingwa wa miaka nyingi Namibia, ambao walilemewa na Kenya 21-18 katika fainali ya 2019, wako katika orodha ya mataifa saba ta kigeni yanayokuja Kenya.

Kikosi cha Chipu cha maandalizi ya Barthes Trophy 2022:

Anthony Dimba, Stanislaus Shikholi, Joseph Ayiro, Raymond Chacha (Strathmore Leos), Mathias Osimbo (Sigalagala), Cornelius Mokoro, Wilhite Mususi, Vincent Omondi, Patrick Nyaga, (Kenya Harlequin), Pesian Elvis Kolian, Roy Mulievi, Tyson Juma Maina, Tony Owino Oketch (Menengai Oilers), Charles Odhiambo Omoro (Nondescripts), Samuel Mwaura (Topfry Nakuru), Felix Chacha (Mwamba), Paywick Munoko (Masinde Muliro), Bill Abuom, Brian Makaya (Mean Machine), David Mwangi (Laiser Hill), John Baraka (Kabras Sugar), Gilbert Ogutu, Craig Odhiambo, Anderson Oduor (Impala Saracens), Solomon Maleu, Allan Zaddock, Malvin Nganga (Homeboyz), Laban Kipsang (Eldoret), Augustine Owino, Meshack Ochieng, Randy Odhiambo, Emmanuel Opondo (Daystar Falcons), Brian Otieno (Comras), Idd Gaguma, Adnan Juma (South Coast Pirates) na Nicholas Otieno Okullo (Blak Blad). Kocha mkuu – Curtis Olago.