Connect with us

General News

Timamy aapa kurejesha tamasha za kitamaduni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Timamy aapa kurejesha tamasha za kitamaduni – Taifa Leo

Timamy aapa kurejesha tamasha za kitamaduni

NA KALUME KAZUNGU

GAVANA wa zamani wa Lamu, Issa Timamy ameapa kurudisha tamasha zote za utamaduni zilizokuwa zikiadhimishwa kila mwaka eneo hilo iwapo atachaguliwa katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Tamasha hizo ambazo zilikuwa kivutio kikuu cha watalii ni pamoja na Utamaduni wa Lamu, maonyesho ya chakula, mashindano ya kila mwaka ya uvuvi, Maulid ya Lamu, Yoga na nyinginezo.Hafla hizo zilikuwa zimeugeuza mji wa Lamu na kuupa jina la ‘Kisiwa cha Tamasha’.

Kwa zaidi ya miaka mitano sasa, nyingi ya tamasha hizo hazijaadhimishwa Lamu, hali ambayo gavana huyo wa zamani aliitaja kulemaza juhudi za kuukuza, kuutangaza na kuuza utalii wa eneo hilo kwenye mataifa ya nje. Bw Timamy alimlaumu mrithi wake, Fahim Twaha, kwa kutowajibikia kuendelezwa kwa tamasha hizo alizozitaja kuwa muhimu kwa wakazi wa Lamu.

“Huyu gavana wenu ameshindwa kabisa kuendeleza tamasha za Lamu ambazo husaidia kukuza utalii eneo hili. Isitoshe, mji wa Lamu ni mchafu. Mnipigie kura ili kuniwezesha kurejesha hizi sherehe. Kwanza mkinichagua niko tayari kuanza kuadhimisha Tamasha za Utamaduni wa Lamu Novemba mwaka huu,” akasema Bw Timamy.

Kiongozi huyo wa zamani pia aliahidi kufufua uvuvi wa Lamu ambao alidai umesambaratika.Pia aliwaahidi wananchi kutatua migogoro iliyokithiri ya ardhi na kupiga jeki kilimo na ufugaji eneo hilo.

“Uvuvi ni uti wa mgongo kwa uchumi wa Lamu. Nikichaguliwa nitahakikisha sheria zote zinazokandamiza wavuvi wetu baharini zinatupiliwa mbali. Pia nitasukuma ardhi zipimwe na wananchi wetu wapate makao,” akasema Bw Timamy.

Pia aliahidi kuimarisha miundomsingi ya afya ambayo alidai imelemazwa na mrithi wake.

“Hospitali hazina dawa. Nikiingia madarakani nitasawazisha mambo hayo ili wananchi wapate huduma bora za afya kwani ni haki yao,” akasema Bw Timamy.

Bw Timamy wa chama cha ANC tayari ameidhinishwa na mrengo wa Kenya Kwanza kuipeperusha bendera ya ugavana wa Lamu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti 9, 2022.

Atapambana na mpinzani wake mkuu, ambaye ni gavana wa sasa, Fahim Twaha (Jubilee), Naibu wa zamani wa gavana, Eric Mugo (Narc Kenya) na mwanamke wa kipekee kwenye kinyang’anyiro hicho, Umra Omar wa chama cha Safina.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending