Connect with us

General News

Wakazi 200 wajitokeza kwa upanzi wa miti kuhifadhi vyanzo vya maji kijijini Athena – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakazi 200 wajitokeza kwa upanzi wa miti kuhifadhi vyanzo vya maji kijijini Athena – Taifa Leo

Wakazi 200 wajitokeza kwa upanzi wa miti kuhifadhi vyanzo vya maji kijijini Athena

NA LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa kijiji cha Athena kaunti ya Kiambu, wamehimizwa kuzingatia upanzi wa miti ili kuhifadhi mazingira.

Bi Jane Kamunge anayejipambanua kama mdau muhimu wa elimu mjini Thika mnamo Jumatatu aliongoza wakazi 200 kwa upanzi wa miti siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani. Imeadhimishwa leo Jumanne, Machi 22, 2022.

Bi Kamunge ambaye anawania kiti cha ubunge Thika, aliwahimiza wakazi hao wawe mstari wa mbele kuzingatia kilimo kwa sababu wanaishi karibu na chemchemi ya maji.

Vile vile aliwahimiza wajitahidi kufuga samaki.

“Nyinyi wakazi wa Athena mna bahati kubwa kuwa na chanjo kikubwa cha maji. Kuna haja pia ya nyinyi kufuga samaki kwa wingi ili iwe kama akiba ya kuzuia njaa siku za usoni,” alifafanua Bi Kamunge.

Zaidi ya miche 500 ilipandwa katika kijiji hicho.

Bi Kamunge aliwahakikishia wakazi hao kuwa atafanya juhudi kuona ya kwamba Wizara ya Kilimo inafanya hima kuona ya kwamba wakazi hao wanapata ujuzi wa kufuga samaki na pia kuchimba vidimbwi kadha kwa shughuli hiyo.

Bw James Kariuki ambaye pia ni mchungaji wa kiroho, aliwashauri wakazi hao wazingatie kilimo hasa kupanda vyakula vinavyoweza kunawiri kando ya chanzo kikubwa cha maji kilicho katika eneo hilo.

Aliwahimiza kupanda nyanya, vitunguu, na maharage ambayo yanaweza kunawiri mahali hapo.

Bw Kariuki, alieleza watashirikiana na Bi Kamunge, kuona ya kwamba wakazi hao wanafanikiwa katika kilimo.

“Eneo la Athena lina mchanga wa rutuba nzuri kando ya chemchemi ya maji. Kwa hivyo wakazi wa eneo hili hawana budi kujituma,” alieleza Bw Kariuki.

Naye mkazi Bw Leonard Kinoti alisema kukosekana kwa fedha za kutosha kunawanyima fursa ya kupiga hatua katika kilimo kijijini Athena.

“Lau tutapata usaidizi kutoka kwa hazina ya Uwezo Fund, bila shaka tutaweza kupanda sukumawiki, vitunguu, na hata nyanya kando ya chemchemi ya maji. Fedha ndiyo shida kwa upande wetu,” alisema Bw Kinoti.

Alisema kwa wakati huu kuna wakazi 100 ambao wanafuga mbuzi wa maziwa na ufugaji huo umewasaidia kwa kiwango fulani.

Naye mkazi mwingine Bi Mary Siengo ambaye ni mkazi wa kijiji hicho anasema iwapo wataungana pamoja kama wakazi wa hapo wataweza kuendesha kilimo cha hali ya juu.

“Kile tunachohitaji kwa sasa ni fedha za kutupiga jeki ili tujiendeleze katika kilimo,” akasema Bi Siengo akihimiza uwepo wa wataalam wa kilimo wazuri mashinani wanaoweza kuwapa wakazi ujuzi wa kujiendeleza katika kilimo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending