Connect with us

General News

Wanaotaka Junet atupwe nje na Raila wana wivu tu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanaotaka Junet atupwe nje na Raila wana wivu tu – Taifa Leo

ODONGO: Wanaotaka Junet atupwe nje na Raila wana wivu tu

Na CECIL ODONGO

BAADHI ya viongozi wa ODM kutoka eneo la Nyanza wanaongozwa na wivu na ukabila kwa kumtaka kinara wao Raila Odinga amwondoe Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed kama mwandani wake uchaguzi wa mkuu wa 2022 unapokaribia.

Wiki jana, Bw Mohamed alitoa matamshi tata katika mkutano moja wa kisiasa Kaunti ya Nyamira ambapo alidai kuwa serikali itakuwa ya watu wa Nyanza endapo Bw Odinga atafanikiwa kutwaa uongozi wa nchi.

Ingawa tamko hilo lilifasiriwa vingine na wafuasi wa Naibu Rais Dkt William Ruto kuwa utawala wa Bw Odinga huenda ukawa wa Waluo pekee, wabunge wa ODM ndio wangekuwa mstari wa mbele kumtetea badala ya kumkashifu.

Si siri kuwa kuna imani au dhana hapa nchini kuwa kabila linalotoa mshikilizi wa kiti cha Urais, hunufaika kuliko makabila mengine.

Hii ndiyo maana Wakenya kutoka maeneo mengine hufikiria kuwa Mlima Kenya ambayo imetoa Marais wawili na Bonde la Ufa, ni kati ya maeneo ambayo yameshuhudia maendeleo tele.

Kwa hivyo, Bw Mohamed hafai kusulubishwa kwa kusema ukweli licha ya hofu kuwa huenda makabila mengine yakaingia uoga na kukosa kumchagua Bw Odinga 2022.

Kulikuwa na habari kuwa kutokana na tamko hilo, Bw Mohamed hakuandamana na Bw Odinga katika ziara yake jijini Kisumu huku madai yakishamiri kuwa baadhi ya wanasiasa walikuwa wamepanga mbunge huyo azomewe kwa ‘kumharibia’ Bw Odinga kura.

Kwanza, eneo la Nyanza limekuwa likizingatia sana demokrasia na kuwachagua wanasiasa ambao baadhi hawatoki jamii ya Waluo.

Kando na Bw Mohamed ambaye amewahi hata kuhudumu kama Meya wa Migori, mbunge wa Kisumu Mjini Mashariki Shakeel Shabir amekuwa akipigiwa kura na sasa anahudumu kipindi chake cha tatu bungeni.

Licha ya kuchezewa shere katika mchujo wa ODM 2017, Bw Shabir alichaguliwa kama mwaniaji huru kwa msingi wa utendakazi wake kwa raia wala si kutokana na kabila lake.

Kwa hivyo, shinikizo za kumtaka Bw Odinga amteme Bw Mohamed kutamsawiri vibaya kinara huyo wa upinzani kama kiongozi wa kikabila hasa wakati huu anapopigania kuingia ikulu 2022.

Pia Bw Odinga ana tajriba pevu ya kisiasa na anafahamu wanasiasa ambao anafaa kuwaamini ndiposa katika baadhi ya mikutano muhimu hasa ya kisiri, amekuwa akiandamana na mbunge huyo.

Mnamo Machi 31, 2018 wakati alipoamua kuzika tofauti yake ya kisiasa na Rais Uhuru Kenyatta kupitia ‘handisheki’, Bw Odinga alikuwa ameandamana na Junet pekee.

Pia katika ziara zake za nje na ikuluni, Bw Odinga amekuwa akiandamana na Kiranja huyo wa Wachache Bungeni na hili linadhihirisha kuwa huenda anafahamu mambo mengi ambayo wanasiasa hawa hawayafahamu.

Aidha, baadhi ya wanasiasa ambao wanalalamika kuwa Bw Mohammed anaiponza au kumharibia Bw Odinga ndio wamekuwa wakishirikiana naye tangu ajitose kwenye siasa mnamo 1992 ila hawajawahi kumsaidia kushinda kiti cha Urais.

Pia baadhi ya wanasiasa hao ambao wanatoka Kaunti ya Migori wanatishiwa na umaarufu wa Bw Mohamed ambaye ametangaza kuwa analenga kiti cha ugavana na sasa wanajaribu kutumia jambo dogo kumpaka tope asifanikiwe 2022.

Badala ya kuchimbiana, huu ndio wakati wa wanasiasa wa ODM kutoka Luo Nyanza kuungana na kuwashawishi raia wajisajili kama wapigakura.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending