Sunday, 8 November 2026
Kenyan Digest

Ragwa ahama UDA, kuwa mwaniaji huru kwa useneta – Taifa Leo

1 min read
Published

Ragwa ahama UDA, kuwa mwaniaji huru kwa useneta

NA ALEX NJERU

MWANIAJI wa Useneta Kaunti ya Tharaka-Nithi, Bw Samuel Ragwa (pichani) ambaye alipoteza kwenye mchujo wa UDA wiki jana, ametangaza kuwa sasa atawania kama mwaniaji huru kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Bw Ragwa alisema hawezi kukata rufaa kuhusu uteuzi huo aliodai ulijaa udanganyifu na kuhujumu demokrasia.

Alibwagwa na Diwani wa Mukothima, Mwenda Gataya aliyepata kura 40,746 .