[ad_1]
Gofu ya Safaricom Tour ya Karen yavutia wachezaji 280
Na GEOFFREY ANENE
RAUNDI ya saba ya mashindano ya gofu ya Safaricom Golf Tour yatafanyika katika klabu ya gofu ya Karen mnamo Mei 13-14.
Imevutia wachezaji 280 kutoka kaunti ya Nairobi na viungani mwake. Raundi hiyo inafuata ile ya sita iliyofanyika mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu majuma mawili yaliyopita. Itafanyika wakati mmoja na hamasisho la gofu ya chipukizi katika klabu hiyo.
“Inafurahisha sana kuandaa shindano letu la saba uwanjani Karen. Nafurahi kuona mashindano haya yakiendelea kutambua, kutafuta na kukuza talanta mpya, hasa katika kiwango cha maeneo. Hii inathibitisha kuwa wengi wa wachezaji wetu chipukizi wanahitaji njia wanayoweza kuonyesha talanta yao,” alisema Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom, Peter Ndegwa.
Mashindano ya Safaricom Golf Tour, ambayo yalianza Januari 2022, yameshuhudia karibu wanagofu 2,000 wakishiriki katika vitengo vya kampuni, makadi na chipukizi. Chipukizi wengine 2,000 pia wamepata mafunzo kupitia hamasisho na miradi ya kuwafikia.
Kufikia sasa, mashindano hayo yamezuru maeneo ya Nanyuki, Limuru, Muthaiga, Nyanza, Machakos na Eldoret.
Safaricom pia imeshirikiana na Wakfu wa Gofu ya Chipukizi (JGF) kuendelea kutambua na kulea talanta changa. Chipukizi wanaweza kujiandikisha katika wakfu hiyo kwa Sh1,000 kupata huduma za gofu katika klabu yoyote nchini.
Next article
Shirika lazindua mpango kushirikisha vijana kutoa huduma za…
[ad_2]
Source link