[ad_1]
Jinsi Kibaki alivyoaibishwa hadharani baada ya kukosana na Moi
NA STEPHEN MUNYIRI
INGAWA amerejelewa kama mwanasiasa mtulivu ambaye alilenga sana maendeleo, marehemu Mwai Kibaki pia alipitia changamoto kisiasa ikiwemo wakati mmoja kuaibishwa hadharani katika mkutano wa Kanu.
Mnamo 1988, punde tu baada ya kutimuliwa kama makamu wa rais na Daniel Moi, Mzee Kibaki aliaibishwa katika kongamano la wajumbe wa KANU katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi alipoondolewa kutoka jukwaa kuu na kulazimika kuketi pamoja na wajumbe wa Nyeri.
Kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa Mzee Kibaki, Bw Joe Wanjau, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Nairobi Fred Waiganjo alimwendea Mzee Kibaki aliyekuwa ameketi jukwaani na kumwambia alikuwa ameamrishwa asimruhusu aketi hapo.
Hii ni licha ya kuwa Mzee Kibaki bado alikuwa makamu mwenyekiti wa KANU hata baada ya kuondolewa kama makamu wa rais.
“Habari za asubuhi bwana waziri. Nimeamrishwa nikujulishe kuwa hufai kuketi katika jukwaa kuu. Unafaa uketi mahala ambapo pametengewa wajumbe wa Kanu kutoka Nyeri,” akasema Bw Wanjau.
Kwa mujibu wa Bw Wanjau, Mzee Kibaki alitii na kutembea polepole kutoka jukwaa kuu akiwa mtulivu kisha akaketi miongoni mwa wajumbe wa Kanu waliotoka Nyeri.
“Hakuna shida si kiti ni kiti,” alisema Mzee Kibaki wakati huo.
Inadaiwa kuwa masaibu ya Mzee Kibaki yalitokana na hatua yake ya kususia mkutano wa baraza la mawaziri uliokuwa umeitishwa na Moi.
Next article
TAHARIRI: Serikali sharti itatue hili suala la mafuta…
[ad_2]
Source link