Connect with us

General News

Korti yaokoa mzazi kumpeleka mtoto katika shule ghali – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Korti yaokoa mzazi kumpeleka mtoto katika shule ghali – Taifa Leo

Korti yaokoa mzazi kumpeleka mtoto katika shule ghali

NA BRIAN OCHARO

MAHAKAMA ya masuala ya familia Mombasa imeamua kuwa wazazi hawastahili kulazimishwa kulipia mambo wasiyoweza kugharimia, wanapowajibika kutimiza haki za watoto.

Akitoa uamuzi katika kesi ambapo mwanamume alishtakiwa kwa kutomlipia mtoto wake karo katika shule ya kibinafsi, Jaji John Onyiego alisema ushahidi ulionyesha kuwa baba huyo hana uwezo wa kusomesha mtoto katika shule ambayo mkewe wa zamani alitaka.