Connect with us

General News

Ramadhani inatuumiza, wauza miraa sasa walia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ramadhani inatuumiza, wauza miraa sasa walia – Taifa Leo

Ramadhani inatuumiza, wauza miraa sasa walia

NA KALUME KAZUNGU

WAFANYABIASHARA wa miraa, Kaunti ya Lamu wamelalamikia kudidimia kwa biashara hiyo tangu Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ulipoanza mapema Aprili 2022.

Waraibu wengi wa miraa hupatikana kisiwa cha Lamu na miji ya Mokowe, Witu na Kiunga, ambapo idadi kubwa yao ni waumini wa dini ya Kiislamu.

Wateja hao kwa sasa wameadimika kwenye vibanda vya miraa kwani huwa wako kwenye saumu mchana kutwa.

Akizungumza na Taifa Leo jana Jumapili, Mwenyekiti wa Wachuuzi wa Miraa, Kaunti ya Lamu, Ibrahim Kamanja, alisema biashara ya miraa imeshuka kwa karibu asilimia 50 tangu Ramadhani ilipong’oa nanga.

Bw Kamanja alisema bei ya miraa pia imeenda chini kutokana na uchache wa wanunuzi.

“Wachuuzi wa miraa tunaumia. Awali ulikuwa ukiuza miraa yako ya hadi Sh30,000 kwa siku. Tangu Mwezi wa Ramadhani uanze, wateja wamepungua pakubwa. Mchana waweza kukosa wateja kabisa ilhali jioni, baada ya Waislamu kufungua saumu, waweza ukauza miraa ya kati ya Sh7,000 au Sh8,000 pekee. Hali ni ngumu,” akasema Bw Kamanja.

Mohamed Omar ambaye ni mmiliki wa boti zinazosafirisha miraa kutoka Lamu kuelekea nchi jirani ya Somalia anasema amelazimika kusitisha shughuli zake hadi pale Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utakapofikia ukingoni.

Anasema tangu Ramadhani ilipoanza, biashara ya miraa nchini Somalia pia imeshuka. Uchunguzi wa Taifa Leo ulibaini kuwa nyakati za kawaida, wanabiashara wa miraa kutoka Lamu kuelekea nchini Somalia hutuma kati ya boti 10 hadi 12 kusambaza miraa.

Aidha tangu Ramadhani ianze, boti zinazoelekea nchini Somalia kutoka Lamu kwa minajili ya kusambaza miraa huwa ni mbili au tatu pekee.

“Utaendaje safari hiyo ya mbali na shehena za miraa ambayo haitanunuliwa. Tumeonelea vyema kusitisha kidogo usafirishaji wa miraa kwa wingi nchini Somalia hadi mwezi wa Ramadhani ukamilike,” akasema Bw Omar.

Peter Muriungi alisema kilo ya miraa ambayo huuzwa kwa kati ta Sh3,500 na Sh4,000 kwa sasa wanalazimika kuiuza kwa bei ya chini ambayo ni kati ya Sh2,500 na Sh3,000 pekee. Bw Muriungi anasema kabla ya Ramadhani, pia wamekuwa wakiuza fungu la miraa ya mwananchi wa kawaida kwa kati ya Sh500 na Sh600.

Hata hivyo anasema tangu Ramadhani ianze, wamelazimika kuuza mafungu hayo ya kawaida ya miraa kwa bei ya chini ambayo ni kati ya Sh200 na Sh300 pekee.

“Matumaini yetu ni kwamba punde Ramadhani itakapofikia ukingoni, hali itarejea kuwa ya kawaida. Tunaelewa kabisa kwamba wenzetu wako kwenye mfungo wa Ramadhani. Huu msimu ukikamilika mambo yatakuwa shwari kibiashara,” akasema Bw Muriungi.