Connect with us

General News

441 kukosa matokeo ya KCSE sababu ya udanganyifu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

441 kukosa matokeo ya KCSE sababu ya udanganyifu – Taifa Leo

441 kukosa matokeo ya KCSE sababu ya udanganyifu

NA MARY WANGARI

JUMLA ya wanafunzi 441 waliofanya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) 2021 ikiwemo watahiniwa wote katika kituo kimoja watakosa matokeo yao baada ya Wizara ya Elimu kufutilia mbali matokeo hayo kuhusiana na udanganyifu.

Taarifa iliyotolewa na Profesa George Magoha, iliashiria kuwa visa vya udanganyifu katika mtihani wa KCSE 2021 viliongezeka kwa visa 154 zaidi na kufikia jumla ya visa 441, ikilinganishwa na jumla ya visa 287 vilivyorekodiwa 2020.

Idadi ya wanafunzi walionaswa wakitumia simu kudanganya kwenye mitihani hiyo iliongezeka zaidi ya maradufu katika KCSE 2021 na kufikia jumla ya 223 ikilinganishwa na visa 45 pekee mnamo 2020.

Visa vya watu walionaswa wakijifanya watahiniwa viliongezeka hadi watu wanane katika KCSE 2021 ikilinganishwa na mtu mmoja katika KCSE 2020.

Visa vya usambazaji wa nakala za mitihani kinyume na sheria vilipungua hadi 203 katika KCSE 2021 ikilinganishwa na visa 211 mnamo 2020 huku visa vya watahiniwa kushirikiana kudanganya kwenye mitihani vikipungua kutoka 29 katika mtihani uliopita hadi wanafunzi sita mwaka huu.

Sawa na 2020, kisa kimoja cha kusababisha vurugu kwenye chumba cha mtihani kiliripotiwa katika KCSE 2021 ambacho ni miongoni mwa matokeo yaliyofutiliwa mbali.

“Kabla ya Mtihani wa KCSE 2021 kuanza, serikali iliimarisha mikakati iliyodhamiriwa kukomesha aina yoyote ya udanganyifu kupitia juhudi za pamoja kutoka kwa timu iliyojumisha vikosi mbalimbali. Matokeo ya uangalizi huo ulioimarishwa ni kuwa karibu visa vyote vya udanganyifu ambavyo vingetokea vilizuiwa. Taifa ni shahidi kuwa simu nyingi ambazo zingetumiwa kutuma nakala za mitihani zilikamatwa kabla ya kutumiwa,” alisema Waziri Magoha.

Akitangaza matokeo hayo Jumamosi, Waziri wa Elimu alisisitiza kuwa Baraza la Kitaifa linalosimamia Mitihani Nchini (KNEC) litawachukulia hatua kali za kinidhamu wote waliohusika na visa vya udanganyifu kwenye mitihani mwaka huu.

“Hata hivyo, visa 441 viliripotiwa kwenye Mtihani wa KCSE 2021 na kisa cha kituo kimoja ambapo matokeo yote yanazuiliwa. Nataka kusema wazi kwamba KNEC haitakuwa na huruma yoyote kwa wahusika wa udanganyifu kwenye mitihani ambao ni sharti wachukuliwe hatua ipasavyo. Kwa sababu hiyo, matokeo ya visa vyote 441 yamefutiliwa mbali,” alisema.

Waziri ametoa wito kwa wadau wote wa mitihani ya kitaifa kuunga mkono juhudi za serikai zinazoendelezwa za kukomesha udanganyifu kwenye mitihani.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending