Connect with us

General News

680 kushiriki Riadha za Dunia za Ukumbini, Omanyala anaongoza Wakenya 10 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

680 kushiriki Riadha za Dunia za Ukumbini, Omanyala anaongoza Wakenya 10 – Taifa Leo

680 kushiriki Riadha za Dunia za Ukumbini, Omanyala anaongoza Wakenya 10

NA GEOFFREY ANENE

SHIRIKISHO la Riadha Duniani limetangaza orodha ya wanariadha 680 watakaoshiriki Riadha za Dunia za Ukumbini jijini Belgrade, Serbia mnamo Machi 18-20.

Mshikilizi wa rekodi ya Afrika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala yuko katika orodha ya watimkaji 54 kutoka mataifa 48 yatakayowakilishwa katika mbio za mita 60. Omanyala anajivunia muda wake bora wa mita 60 wa sekunde 6.57 mjini Lievin, Ufaransa mnamo Februari 17.

Baadhi ya majina makubwa katika kitengo hicho cha Omanyala ni pamoja na Waamerika Christian Coleman (6.45) na Marvin Bracy (6.48), bingwa wa Olimpiki mita 100 Mwitaliano Marcell Jacobs (6.47), Emmanuel Matadi kutoka Liberia (6.52) na Arthur Cisse kutoka Ivory Coast (6.53).

Wakenya Collins Kipruto na Noah Kibet watakabiliana na watimkaji 25 kutoka mataifa 17 katika mbio za mita 800 akiwemo Mhispania Mariano Garcia anayejivunia kasi ya juu mwaka 2022 ya dakika 1:45.12.

Katika mbio za mita 1,500, Kenya itawakilishwa na Abel Kipsang atakayebiliwa na kibarua kutoka kwa wakali Jakob Ingebrigtsen (Norway), Samuel Tefera (Ethiopia) na Mhispania Adel Mechaal, miongoni mwa wengine. Kitengo hiki kina watimkaji 37 kutoka mataifa 24.

Daniel Simiu (dakika 7:37.86) na Jacob Krop (7:31.90) wako katika orodha ya wakimbiaji 35 kutoka mataifa 25 watakaowania ubingwa wa mbio za mita 3,000. Waethiopia Berihu Aregawi (7:26.20), Lamecha Girma (7:30.54) na Selemon Barega (7:30.66) ndio wana muda bora kuliko wote katika kitengo hicho.

Kenya itawakilishwa na Eglay Nalyanya na Naomi Korir katika mbio za mita 800 za kinadada ambazo zina watimkaji 20 kutoka mataifa 13 wakiwemo Muingereza Keely Hodgkinson, raia wa Jamaica Natoya Goole na Mganda Halimah Nakaayi.

Beatrice Chebet na Edinah Jebitok watapeperusha bendera ya Kenya mbio za mita 3,000 za kinadada zilizovutia washiriki 21 kutoka mataifa 14.

Kenya ilimaliza makala yaliyopita mjini Birmingham, Uingereza katiak nafasi ya 24 kwa medali moja ya shaba ambayo Bethwell Birgen alishinda katika mbio za mita 3,000.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending