Akifichua hisia zake Instagram, Akothee alisikitika kwamba baada ya wanawe kulala yeye husalia na upweke kwa kukosa mchumba.
“Hizi ndizo zile nyakati ambapo unahisi kweli upweke una machungu. Unamaanisha hata sipokaribu kuonana na mpenzi wangu hivi karibuni? Sasa baada ya watoto kulala, nifanye nini nikiwa pekee yangu? Kwa kweli uhusiano wa mapenzi sio wa kila mtu,” Akothee alidokeza.
Habari Nyingine:
Alitoa mfano wa penzi lake Vanessa na Rotimi ambao walipakia video yao kwenye Instagram wakilishana mahaba na kufichua kuwa anatamani kuwa katika uhusiano sawia na huo.
“Jamani Vanessa mbona unatutesa hivi, subiri mwanzo pia sisi tupate wachumba tufurahie pamoja. Penzi ni tamu,” aliwamiminia sifa wapenzi hao.
Awali penyenye zilisema kuwa Madam Boss alikuwa katika uhusiano wa mapenzi na meneja wake Nelly Oaks.