Connect with us

Entertainment

Lilian Muli afurahia maisha yake

Published

on

– Lilian Muli amepanda ngazi kimaisha tangu aanze safari ya utangazaji katika kituo cha KTN baada ya kumaliza chuo kikuu

– Amekuwa mmoja wa mabinti sugu kwenye usomaji wa runinga humu nchini na kwa sasa anatamba sana

– Alisema maisha yake kwa sasa ni kama filamu huku akiwapa mashabiki nafasi ya kuona gari lake la thamani

Mtangazaji maarufu wa runinga Lilian Muli anaendelea kufurahia maisha yake licha ya kuwa hujipata kwenye sakata mbali mbali.

Muli alianza safari yake ya utangazaji katika kituo cha runinga cha KTN ambapo alitiwa makali na kufikia alipo sasa.

Lilian Muli ajivunia maisha yake, asema ni kama filamu

Lilian Muli na marafiki zake wakijivinjari.

Kwa sasa kipusa huyo mwenye umbo na sura ya kupendeza ni mmoja wa wasomaji habari sugu zaidi wa kike humu nchini.

Ni jambo ambalo wadokezi wameeleza Kenyan Digest kuwa limemfanya awe mmoja wa wanaopata mshahara mkubwa kwenye runinga ya Citizen.

Huku akaunti yake ya benki ikiwa imejaa na kufurika, Muli amekuwa akiishi maisha ya kutamaniwa na wanahabari ambao bado wanatambaa.

Amekuwa hafichi kuwa maisha yake yanapepea na hivi majuzi alichapisha picha moja kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema maisha yake sasa ni kama filamu.

“Maisha ni nini . . . yangu ni kama filamu,” aliandika mwanahabari huyo tajika.

Haikubainika ni kwa namna gani alilinganisha maisha yake na filamu lakini ilikuwa wazi kuwa gari analomiliki si la peni nane.

Comments

comments

Facebook

Trending