” Imebainika kuwa wafanyakazi wetu 2 wamepatikana na virusi vya COVID-19, hata hivyo, tumekuwa tukizingatia masharti yaliowekwa na wizara ya afya ya kudhibhiti maambukizi ya virusi hivyo, ” Alisema Bilal.
Bilal pia aliwashauri wale ambao wametangamana na wagonjwa hao wawili kujitokeza ili wafanyiwe vipimo vya COVID-19 au wajiweke karatini.
Vile vile, wale ambao wanajihisi wagonjwa wameshauriwa kutafuta huduma za daktari iwapo wanahisi dalili zozote za magonjwa yoyote.