Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imetangaza kuwa huduma za M-Pesa zitakosekana kwa muda Jumatatu, Julai 6 kati ya saa tano na dakika hamsini na tisa usiku na Julai Jumanne 7 saa kumi na moja asubuhi.
Kwenye taarifa yake iliyochpaishwa mitandaoni kampuni hiyo ilisema huduma zote za M-Pesa ikiwemo ununuzi wa mjazo wa simu zitasitishwa kwa ajili ya kuboresha mfumo wake.
Wateja hawataweza kutuma wala kupokea pesa wakati wa kuboreshwa kwa mfumo huo. Picha: Roberto Muyela/Tuko.co.ke.. Source: Original
Kwa zaidi ya miaka 13, M-PESA imeendelea kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu nchini Kenya, kwa kuwaunganisha na fursa mpya kila siku. Ili kuboresha zaidi mabadiliko haya, tunafanya ukarabati wa mfumo wetu mara kwa mara,” taarifa hiyo ilisema.
“Kuhusiana na suala hili, huduma zetu za M-PESA zitakuwa zikikarabatiwa Jumatatu, Julai ,6 2020, kati ya saa tano na dakika hamisni na tisa usiku na saa kumi na moja asubuhi.