Afisa wa kike alishtakiwa Jumanne, Julai 7 kwa kosa la kujaribu kuua baada ya kumfyatulia risasi mumewe mara mbili nyumbani kwao mtaani Dago, Nyalenda eneo bunge la Kisumu Mashariki.
Konstebo Maureen Awuor alifikishwa mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama ya Winam, Fatuma Rashid ambapo alikana mashtaka.
Afisa akiwa ameshikilia bunduki ya aina ya AK47. Picha: UGC. Source: UGC
Mahakama iliarifiwa kuwa mnamo Julai 5, 2020, Awuor mwenye umri wa miaka 35 alijaribu kumuua mumewe Victor Odhiambo mwenye umri wa miaka 28 nyumbani kwao.
Iliripotiwa kwamba wachumba hao ambao wamekuwa kwa uhusiano kwa miaka mitatu walikorofishana baada ya jamaa kumpa mfanyikazi wao wa nyumba KSh 50 bila idhini ya mkewe.
Kamanda wa Kisumu Mashariki Mwenda Musyimi alisema kostebo Owuor ambaye anahudumu katika kituo cha Kasagam, alirejea nyumbani na bunduki ya AK47 na kumpiga risasi mbili jamaa, kichwani na kwenye sikio.
Afisa huyo aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu KSh 500,000 au bondi ya KSh 2 milioni.
Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 21, 2020 na kusikizwa Septemba 30.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.