Waziri Mutahi Kagi Alhamisi, Julai 9 alipotangaza visa vipya vya Covid-19. Picha: NTV Source: Facebook
Visa hivyo vilitokana na sampuli 3803 ambazo zilifanyiwa ukaguzi na sasa idadi ya maambukizi Kenya imefikia watu 8975.
Kagwe alitoa ripoti hiyo akiwa katika kaunti ya Mombasa ambapo alisema pia wagonjwa wanne wameangamizwa na makali ya coronavirus.
“Kwa udadisi wetu, ni kama watu 138 kwa sasa wanapatikana na virusi vya Covid-19 kwa kila watu 100,000 Mombasa na watu 100 kwa watu 100,000 Nairobi,” alisema Kagwe.
Kagwe alionya kuwa huenda Mombasa ikaathirika pakubwa kwa sababu watu wengi wamekuwa wakimezea kuzuru eneo hilo kaunti zikifunguliwa.
Mombasa ina visa 1,663 na huenda visa hivi vikaongezeka kwa sababu Mombasa ni mahali kila mtu Nairobi amekuwa akitaka kuzuru kafyu ya kusafiri ikitolewa”, Kagwe alisema.