Miezi michache baada ya kumkomboa mvulana mlemavu, Shadrack Mwita, mwanamziki huyo amegundua kuwa alimdanganya kuwa ni yatima muda huo wote.
Pia alitambua kuwa Shadrack ana bibi ambaye yuko hai na mzima kisiha licha ya kudanganya kuwa alipoteza maisha yake katika ajali na kumuacha pekee yake.
Katika ujumbe uliojaa huzuni kwenye Instagram, msanii huyo anayesifika kwa wimbo Oyoyo alifichua kuwa ametengana na kumsaidia Shadrack kama mbingu na ardhi.
Akothee alikuwa ameanza kumtambua Shadrack kama mtoto wake wa kiume mkubwa.Picha:Akothee. Source: Instagram
Mama huyo wa watoto watano alisema alikuwa anashangazwa na namna mtoto wake wa kuasili alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo kila mara.
“Ilibidi nijifunze kutenganisha udhamini na kutatiza maisha yangu ya faragha na maisha ya familia. Familia ya Shadrack ilijitokeza na nilizidiwa na presha. Kwanzia sasa, Shadrack ana nyumba yake ya kukodisha na kulipiwa kodi ya mwaka mzima,” aliandika Akothee.
Mmiliki huyo wa wakfu ya Akothee Foundation pia aliongezea kuwa licha ya urongo, bado atamfungulia Shadrack biashara ili aweze kukimu familia yake.
Rais huyo wa akina mama wasimbe alikutana na kijana huyo mitaani akielekea dukani.
Alimhoji na kutaka kujua historia yake na kisha wawili hao wakawa na uhusiano dhabiti.
Akothee alianza kwa kumpa chumba kabla ya kumpeleka katika jumba lake la kifahari mjini Mombasa.
Alimvisha, akamlisha na kumuonyesha upendo kabla ya kumnunulia miguu ya vyuma ya kumuwezesha Shadrack kutembea tena.
Akothee hata alishindwa kumshughulikia binti yake ambaye alikuwa anafanyiwa upasuaji ili aweze kuwa karibu na Shadrack wakati anajifunza kutembea.