Otiende Amollo ndiye atahudumu kama mwenyekiti wa kamati ya sheria bungeni. Picha: Otiende Amollo Source: Facebook
Kuria alisema wandani wa Raila walipewa nafasi hizo kama vibaraka wa kuhakikisha malengo ya kigogo wao wa siasa.
Alisema baadhi ya malengo hayo ni kuhakikisha kuwa ripoti ya BBI inapitishwa bungeni ifaavyo na pia kuchaguliwa kwa msajili mpya wa vyama vya kisiasa.
“Sasa msisahau kwa nini Baba amewateua kwenye kamati hii. Ni ili muweze kupitisha BBI, kuchaguliwa wa Jaji Mkuu anayependelea Baba, mulete tume huru ya mipaka na uchaguzi inayoegemea upande wake na msajili wa vyama,” alisema Kuria.