Idadi ya walioambukizwa virusi vya COVID- 19 sasa imefikia 11,252 baada ya watu wengine 461 kupatikana na virusi hivyo Jumatano Julai 15
Akiwahutubia wananchi Jumatano, Julai 15, katibu katika wizara ya Afya Rashid Aman alisema watu 51 zaidi wamepona kutokana na virusi hivyo na wameruhusiwa kuondoka hospitalini.
Kwa jumla wagonjwa 3,068 wamepona kutokana na virusi hivyo kufikia sasa.
” Leo sampo 4,261 zimefanyiwa vipimo ambapo watu 461 walipatikana na virusi vya COVID-19, hivyo basi idadi ya walioambukizwa virusi hivi nchini imefikia 11, 252,” Aman alisema.
Aman aliongezea kuwa watu wengine 7 wamefariki dunia kutoka na virusi hivyo na kufanya idadi ya vifo kufikia 209.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.