Imeripotiwa kuwa Lali ameachiliwa huru licha ya mahakama ya Lamu kumpata na hatia ya kuhusika katika mauji ya mpenziwe.
Hata hivyo, Lali alikana mashtaka dhidi yake na alikuwa afanyiwe ukaguzi wa kiakili Alhamisi, Julai 16 kabla ya kujibu mashtaka.
Aliyekuwa mpenzi wa Tecra Muigai aachiliwa huru baada ya DPP kufuta mashtaka dhidi yake Source: UGC
Lali alikamatwa mara kadhaa baada ya kujikanganya na taarifa zake kuhusu kifo cha Tecra, kwa mara ya kwanza alisema mrembo huyo alianguka kwenye bafu kabla ya kubadilisha taarifa kuwa alianguka kutoka kwa ngazi ya nyumba.
Tecra alikuwa akiishi na Lali katika nyumba moja mjini Lamu kabla ya kifo chake.