-Mwendwa alimkumbusha Kirauri namna FKF ilisimama na kampuni ya Sportpesa licha ya kufadhili vilabu vingine vya nchi za kigeni
-Hii ni baada ya FKF kuingia katika makubaliano na kampuni ya mchezo wa bahati nasibu kutoka Nigeria, BetKing
-Shirikisho hilo litapokea KSh1.2 bilioni za ufadhili kwa kipindi cha miezi mitano na vilabu vya KPL kupata KSh8 milioni kila msimu
-Karauri, alishangazwa na namna BetKing ilikimbia Ligi ya Soka ya Nigeria(NPFL) na kuja kufadhili KPL
Kulikuwa na mshawasha mtandaoni siku ya Jumapili, Julai 19, kufuatia vita vya maneno kati ya rais wa Shirikisho la Soka Nchini(FKF), Nick Mwendwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya kamari ya SportPesa, Ronald Karauri.
Karauri alimsuta Mwendwa kwa kuingia katika makubaliano na kampuni ya mchezo wa bahati nasibu kutoka Nigeria, BetKing, ambapo shirikisho hilo litapokea KSh1.2 bilioni za ufadhili kwa kipindi cha miezi mitano.
Mwendwa pia alitangaza kuwa katika mwafaka huo, vilabu vyote vya KPL vitapokea KSh8 milioni kila msimu.
Hata hivyo, Karauri, kupitia Twitter, alishangazwa na namna BetKing ilikimbia Ligi ya Soka ya Nigeria(NPFL) na kuja kufadhili KPL, na kumsuta mwendwa kwa kupendelea BetKing badala ya kampuni za humu nchini kama vile Odibets na Betika.
Mwendwa naye alimkumbusha Kirauri namna FKF ilisimama na kampuni ya Sportpesa licha ya kufadhili vilabu vingine vya nchi za kigeni na kutaja matamshi yake kama yasiyokuwa sawa.
“Si maoni sawa Kapteni!Kutoka kwako na unajua Soka ilikuunga mkono hata wakati ulikwenda kufadhili vilabu vingine kushinda Kenya,” alisema Mwendwa.
Mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier pia alitilia shaka mwafaka huo mpya na kusema kwa sasa timu yake inazingatia mkataba mpya wa ufadhili wa KSh55 milioni kila msimu kutoka kwa kampuni ya Betsafe.
Wakenya pia walichangamkia mjadala na kuwa na haya ya kusema
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.