Connect with us

General News

Lempurkel hatimaye huru kutoka jela – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Lempurkel hatimaye huru kutoka jela – Taifa Leo

Lempurkel hatimaye huru kutoka jela

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Mbunge wa Laikipia kaskazini Mathew Lempurkel(pichani) anayetumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kumchapa mbunge wa sasa Bi Sarah Korere jana aliachiliwa kwa dhamana ya Sh100,000 pesa tasilimu.

Bw Lempurkel sasa atasherehekea siku kuu ya krismasi na mwaka mpya pamoja na familia yake kufuatia agizo hilo la Jaji Momanyi Bwonwong’a.

Jaji Bwonwong’a alimwachilia mwanasiasa huyo aliyefungwa miezi miwili iliyopita na hakimu mwandamizi Bi Florence Onkwani.

Jaji huyo alimwamuru Lempurkel awe akipiga ripoti naibu wa msajili wa mahakama kuu mara moja kila mwezi hadi rufaa aliyowasilisha itakaposikizwa na kuamuliwa.

Akitoa uamuzi wa dhamana , jaji huyo alisema rufaa aliyokata Lempurkel inazua masuala mazito ya kisheria.

Pia alisema iko na uwezekano mkubwa wa kubatilisha kabisa uamuzi huo wa Bi Onkwani.

Mahakama iliamuru ushahidi uliowasilishwa mbele ya Bi Onkwani upigwe chapa upesi ndipo rufaa iweze kusikizwa na kuamuliwa bila kuharibu wakati.

“Nakubaliana na wakili Kanchori kwamba rufaa hii ya Lempurkel inaweza kuchukua muda mrefu kusikizwa na kuamuliwa. Sasa naamuru mfungwa huyu aachiliwe kwa dhamana ya Sh100,000 pesa tasilimu kama alivyokuwa amepewa na hakimu,” Jaji Bwonwong’a aliamuru.