Connect with us

General News

Sekta ya kilimo yaendelea kuwa na mchango mkubwa wa kubuni nafasi za ajira – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sekta ya kilimo yaendelea kuwa na mchango mkubwa wa kubuni nafasi za ajira – Taifa Leo

Sekta ya kilimo yaendelea kuwa na mchango mkubwa wa kubuni nafasi za ajira

Na SAMMY WAWERU

ZAIDI ya asilimia 50 ya nafasi za ajira nchini Kenya imebuniwa kupitia sekta ya kilimo.

Takwimu hizi zimetolewa na Shirika la Kilimo na Kuangazia Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika (ACRE), ambalo hutoa huduma za bima ya mimea kwa wakulima wa mashamba madogo.

Kufikia sasa, kaunti tisa zinaridhia bima ya ACRE.

Zinajumuisha Nandi, Bungoma, Makueni, Machakos, Uasin-Gishu, Nakuru, Meru, Embu na Tharaka Nithi.

Kulingana na shirika hilo, kufikia mwishoni mwa mwezi huu, Januari, wanalenga kusambaza huduma za bima ya mimea kwa zaidi ya kaunti 22.

“Sekta ya kilimo Kenya, imebuni zaidi ya asilimia 50 ya nguvukazi,” akasema Bw Ewan Wheeler, Afisa Mkuu Mtendaji ACRE akizungumza jijini Nairobi.

Afisa huyo pia alisema sekta ya kilimo nchini, licha ya changamoto zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, inaendelea kuimarika kiasi cha kuchangia ukuaji wa uchumi kwa zaidi ya asilimia 30, kwa njia ya moja kwa moja.

“Haja ipo wakulima wapigwe jeki kwa kiasi kikubwa,” Bw Wheeler akahimiza.

Ushuru (VAT) wa juu unaotozwa pembejeo; mbegu, fatalaiza na dawa dhidi ya magonjwa na wadudu, unaendelea kutishia jitihada za wakulima.

Isitoshe, serikali inahujumu wanarazaa kwa kuwawekelea mzigo mwingine wa ushuru kupitia gharama ya juu ya mafuta wanaposafirisha mazao sokoni.

Bidhaa za mafuta ya petroli, zilianza kutozwa VAT ya asilimia 8.

Mwaka uliopita, gharama ya petroli, dizeli na mafuta ya taa iliongezeka kwa kiwango kikuu, wengi wa wakulima wakitegemea mafuta ya petroli na dizeli kuendeleza shughuli za ukuzaji wa mimea.

“Mazao yataongezeka maslahi ya wakulima yakiangaziwa,” Wheeler akasema.

Baadhi ya nchi zilizoimarika katika shughuli za kilimo kama vile Denmark na Netherlands, serikali za mataifa hayo zimefanya mazingira ya wakulima kuwa nafuu, kwa kupunguza ushuru unaotozwa pembejeo na bidhaa za kilimo.

Katibu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki – Kenya, Dkt Kevit Desai, pia anahisi haja ipo maslahi ya wakulima kutathminiwa na kufanywa kuwa bora.

Aidha, afisa huyu anakiri sekta ya viwanda inategemea kilimo na ufugaji, kwa kiasi kikubwa.

“Asilimia 50 ya viwanda inategemea sekta ya kilimo, mikakati kabambe,” Dkt Desai asema, akihimiza mikakati kabambe kuwekwa kuiimarisha.

Sekta ya kilimo yaendelea kuwa na mchango mkubwa Kenya kubuni nafasi za ajira.