[ad_1]
Wajackoyah aahidi kuhalalisha chang’aa akiwa rais
Na WINNIE ATIENO
KIONGOZI wa chama cha Roots Prof George Wajackoyah (pichani) ameahidi kuhalalisha chang’aa na kuchunguza upya mkataba kati ya Kenya na China kuhusu reli ya kisasa (SGR) siku 100 za kwanza uongozini akichaguliwa rais.
Alipuuzilia mbali azma ya kinara wa ODM Raila Odinga na mwenzake William Ruto ambao wanamenyania urais akiwataja kama watu ambao hawawezi kusuluhisha changamoto za Wakenya.
Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli moja Mombasa, Prof Wajackoyah alimtaka Bw Odinga aache siasa akisema amekuwa siasani kwa miaka na mikaka.
Alisema SGR imeua biashara za malori eneo la Pwani na akichaguliwa uongozini atahakikisha wafanyibiashara waliowekeza kwenye sekta hiyo wanapata faida kama hapo zamani.
[ad_2]
Source link