Connect with us

General News

Jubilee na ODM havijafanya chaguzi za viongozi wapya kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jubilee na ODM havijafanya chaguzi za viongozi wapya kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Jubilee na ODM havijafanya chaguzi za viongozi wapya kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita

KWA mujibu wa Sheria ya Vyama vya Kisiasa, vyama hivyo vinapaswa kufanya chaguzi za viongozi wapya, kuanzia mashinani hadi ngazi ya kitaifa, kila baada ya miaka mitano.

Endapo chama chochote cha kisiasa kitafeli kutii hitaji hili la kisheria, Msajili wa Vyama vya kisiasa ana mamlaka ya kukifutilia mbali.

Kwa hivyo, Msajili wa vyama vya kisiasa Bi Anne Nderitu asije akasahau kuwa vyama vya Jubilee na ODM vinavyoandaa makongamano ya kitaifa ya wajumbe wao (NDCs) leo havijafanya chaguzi za viongozi wapya kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Kwa mfano, chama cha Jubilee kilichobuniwa mnamo 2016 hakijawahi kufanya uchaguzi wa viongozi wake wa kitaifa.

Viongozi wa sasa wakiongozwa na Katibu Mkuu Raphael Tuju wamekuwa wakishikilia nyadhifa hizo kama “makaimu” kwa miaka sita sasa.

Na mara ya mwisho, ODM kujaribu kuandaa uchaguzi wake ilikuwa Aprili 14, 2014, shughuli hiyo ilipotibuliwa na wahuni waliojulikana kama “Men in Black”.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending