[ad_1]
Viongozi wataka KRA, Keroche kushauriana kuifungua kampuni hiyo
NA MACHARIA MWANGI
VIONGOZI mbalimbali na wafanyabiashara Nakuru wametoa wito kwa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA) kushirikiana na wasimamizi wa Keroche Breweries ili kuifufua kampuni hiyo.
Mwenyekiti wa muungano wa vijana katika kaunti hiyo, Stephen Mungai Kariuki, alishutumu KRA akisema ndiyo imefilisisha kampuni hiyo.
Alisema wengi walitegemea kampuni hiyo na ndio maana kuna haja ya kuifufua.
“Zaidi ya wafanyakazi 250 walitegemea kampuni ya Keroche Breweries. Baadhi yao sasa wanashindwa hata kujikimu,” akasema Bw Kariuki.
Kwa upande mwingine, alitoa wito kwa wanasiasa ambao wanauza sera zao kwa wananchi waingilie kati ili kuifufua kampuni hiyo.
“Ni kinaya kuwa chama tawala cha Jubilee kimeshindwa kuifufua kampuni hii. Kadhalika, chama hicho kimeshindwa kukuza nafasi za ajira zilizoko. Itakuwa vigumu sana kuwashawishi wananchi ikiwa wanasiasa walio uongozini wameshindwa kuifufua kampuni ambayo inategemewa na wengi,” akasema Bw Kariuki.
Alishutumu gavana wa Kaunti ya Nakuru, Lee Kinyanjui, seneta Susan Kihika na wabunge wengine wa kaunti hiyo kwa kukosa kuingilia kati suala hilo.
“Viongozi wetu wanafaa kuwajibika. Wananchi waliowapigia kura wanateseka huku wamenyamaza,” akasema.
Next article
Kura: Mchujo katika ODM utakuwa huru – Mbadi
[ad_2]
Source link