Connect with us

General News

Ashtakiwa kwa madai ya kuiba Sh4.9m za mwajiri wake – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ashtakiwa kwa madai ya kuiba Sh4.9m za mwajiri wake – Taifa Leo

Ashtakiwa kwa madai ya kuiba Sh4.9m za mwajiri wake

NA JOSEPH NDUNDA

MWANAMUME alishtakiwa Jumatatu kwa kuhamisha pesa kutoka akaunti ya benki ya mwajiri wake hadi yake binafsi.

Bw Martin Muriungi alikabiliwa na shtaka la kuiba Sh4.9m za kampuni ya Direct Pay Limited akiwa afisa wa uhusiano wa wateja wa kampuni hiyo.

Shtaka lilisema kwamba alitenda kosa hilo kati ya Februari 20 na Agosti 26 2021 katika afisi za kampuni hiyo zilizoko Kilimani, Nairobi.

Muriungi alikanusha shtaka mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Kibera Charles Mwaniki.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni na mdhamini wa kiasi sawa au alipe Sh500,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa Machi 14.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending