Connect with us

General News

Serikali itekeleze sheria zote za nchi licha ya kampeni kuchacha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali itekeleze sheria zote za nchi licha ya kampeni kuchacha – Taifa Leo

DOUGLAS MUTUA: Serikali itekeleze sheria zote za nchi licha ya kampeni kuchacha

NA DOUGLAS MUTUA

TUMEINGIA katika awamu ya kupendeza katika msimu huu wa siasa. Mambo utakayoshuhudia na kusikia kati ya sasa na Uchaguzi Mkuu wa Agosti yatakushangaza.

Tayari yameanza kushangaza; unafiki wa wanasiasa unajitokeza wazi, kila mmoja akijaribu kukusadikisha kwamba ndiye bora zaidi. Wewe umegeuka mtu muhimu sana hivi kwamba, kila mwanasiasa anaposema neno au kupiga hatua yoyote, ni sharti ajiulize utahisi vipi, athari ni chanya au hasi.

Kila kitu kinatazamwa kwa darubini ya siasa, na kila hatari ya kupoteza kura inaepukwa kama ukoma. Afadhali mambo yaende tenge na kura zipatikane.

Kwa mfano, Rais Uhuru Kenyatta juzi ametoa amri wakora wa bodaboda, ambao wamekuwa wakitunyanyasa kana kwamba nchi hii ni yao peke yao wadhibitiwe.

Agizo hilo lilitokana na kisa ambapo mwanadiplomasia wa kike kutoka Zimbabwe alivuliwa nguo na kudhulumiwa kimapenzi na wahuni hao alipomgonga na kumvunja mguu mmoja wao kwa gari. Ghafla bin vuu, polisi waliku –

wa barabarani wakihangaisha wahudumu wa bodaboda, hata wasiokuwa na hatia. Ilibidi wengi wanywee kabisa, wafiche pikipiki zao na kulalia mate kwa hofu ya kukamatwa, kutupwa jela au kutozwa faini ambazo wao na koo wao hawangemudu.

Alipotoa amri hiyo, Bw Kenyatta aliwatahadharisha wanasiasa dhidi ya kuingiza siasa katika suala hilo kwa maana huu ni wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hata kabla ya mate hayo kumkauka kinywani, Naibu Rais, Dkt William Ruto, alikuja juu na kusema wahudumu wa bodaboda pia ni watu, watendewe haki.

Akisema kila sekta ina wahuni na kusisitiza walengwe wao, Dkt Ruto alitoa mfano wa waovu walio serikalini na kuuliza iwapo serikali inapaswa kuvunjwa kwa sasabu yao. Na kwa kuwa huu ni wakati wa siasa, na ni lazima mpiga kura abembelezwe, agizo la Rais liliondolewa

kwa muda ili, bila shaka, wahudumu wa bodaboda wasimwone Dkt Ruto kama mwokozi wao na kumpa kura.

Sasa inaonekana Dkt Ruto, ambaye anawania urais kwa tiketi ya Muungano wa Kenya Kwanza, ameamua kuisukuma serikali zaidi kuhusu suala hilo. Amewahimiza wahudumu wa bodaboda ambao pikipiki zao zilitwaliwa na polisi wakati wa msako uliotokana na agizo la rais waziendee vituoni!

Huo bila shaka ni uchochezi, yaani kuwaambia watu wafike vituoni vya polisi na kudai pikipiki zao, lakini Dkt Ruto hawezi kufanyiwa chochote kwa kuwa ni wakati wa kampeni.

Huu ndio wakati wa Rais Kenyatta kuonyesha msimamo imara kama kiongozi, atende linalofaa bila kuwafurahisha watu kwa sababu za kampeni ambazo zinapita upesi.

[email protected]