[ad_1]
Chuo Kikuu cha Egerton sasa kuendesha mitihani ya uanasheria
NA KENYA NEWS AGENCY
BAZALA la Mafunzo ya Uanasheria (CLE) limejumuisha Chuo Kikuu cha Egerton katika orodha ya taasisi za elimu ya juu ambazo zitasimamia mitihani ya wanafunzi wa taaluma hiyo.
Afisa Mkuu Mtendaji wa baraza hilo Wambua Kituku alisema kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, mitihani hiyo itafanywa nje ya Nairobi katika bewa kuu la chuo hicho, Njoro, Nakuru, kuanzia Machi 31, 2022.
Dkt Kituku alisema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za baraza hilo kugatua uendeshaji wa mtihani huo ambao hufanyika katika Chuo cha Mafunzi ya Uanasheria (KSL), Bomas of Kenya, Bewa la Karen la Chuo Kikuu cha Kiteknojolia na Kilimo cha Jomo Kenyatta, miongoni mwa vituo vingine.
[ad_2]
Source link