Connect with us

General News

Ukachero wa Kabogo ndani ya Kenya Kwanza – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ukachero wa Kabogo ndani ya Kenya Kwanza – Taifa Leo

SOKOMOKO WIKI HII: Ukachero wa Kabogo ndani ya Kenya Kwanza

NA LEONARD ONYANGO

NAIBU wa Rais William Ruto alipomnasa aliyekuwa Gavana wa Kiambu William Kabogo, ilikuwa habari njema kwa wafuasi wa Kenya Kwanza.

Bw Kabogo alikuwa miongoni mwa wanasiasa wenye tajriba kutoka eneo la Mlima Kenya walionaswa na Dkt Ruto wakati wa mkutano wake aliofanya Machi 13 katika uwanja wa Thika, Kaunti ya Kiambu.

Katika mkutano huo Bw Kabogo alijitawaza kuwa msemaji wa Mlima Kenya huku akisema: “Rais Uhuru Kenyatta aende apumzike taratibu. Nilisikia wakisema hakuna Mkikuyu wa kuzungumzia Wakikuyu… nasema ni mimi nitazungumza.”

Kiongozi huyo wa chama cha Tujibebe Wakenya alionekana kuleta nguvu mpya katika kampeni za Dkt Ruto.

Lakini wiki mbili baadaye, Bw Kabogo ametoa orodha ndefu ya matakwa ambayo anataka Naibu wa Rais kuyatekeleza la sivyo waachane.

Kulingana na Bw Kabogo, Bw Ruto hajatoa mwongozo kuhusu ajenda yake ya maendeleo katika eneo la Mlima Kenya.

Bw Kabogo alimtaka Naibu wa Rais kutekeleza baadhi ya mambo yaliyomo ndani ya Mswada wa Marekebisho ya Katiba (BBI) unaopingwa vikali na Dkt Ruto.

Kabogo anataka kuhakikishiwa na Dkt Ruto kwa njia ya maandishi kwamba atatekeleza atakayoahidi wakazi wa Mlima Kenya.

Je, Bw Kabogo ni kachero wa Azimio ndani ya Kenya Kwanza au ni anatekeleza majukumu yake ya usemaji wa eneo la Mlima Kenya?

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending