Connect with us

General News

Serikali ilipe kampuni za mafuta kuondoa mahangaiko ya uhaba wa bidhaa hiyo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali ilipe kampuni za mafuta kuondoa mahangaiko ya uhaba wa bidhaa hiyo – Taifa Leo

CHARLES WASONGA: Serikali ilipe kampuni za mafuta kuondoa mahangaiko ya uhaba wa bidhaa hiyo

NA CHARLES WASONGA

MAFUTA ni bidhaa muhimu katika uendeshaji wa shughuli muhimu katika sekta zote za uchumi wa nchi hii.

Kwa mfano, bila mafuta sekta muhimu ya uchukuzi itaathirika sawa na ile ya uzalishaji bidhaa na utoaji huduma muhimu.

Watu hawataweza kufika kazini na uchumi unaweza kukwama kabisa.

Matokeo yake ni kwamba taifa linaweza kutumbukia katika lindi la machafuko ikiwa hali hii itaendelea kwa muda mrefu.

Hii ndio maana serikali inafaa kuchukua hatua za haraka kushughulikia kiini cha tatizo la uhaba wa mafuta ambalo linashuhudiwa katika sehemu zote za nchini na hivyo kuwatumbukiza wenye magari na wahudumu wa bodaboda kwenye mahangaiko makubwa.

Imebainika kuwa baadhi ya kampuni za mafuta zimehodhi bidhaa hii kulalamikia hatua ya serikali kuchelewa kuzilipa pesa za kufidia hasara wanazopata kufuatia kuongezeka kwa bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa.

Hazina ya Kitaifa ilifaa kutoa pesa hizo kila mwezi tangu Septemba mwaka jana ambapo bei ya mafuta ilianza kupanda kwa kiwango cha juu zaidi.Lakini juzi muungano wa kampuni za kuuza mafuta nchini (OMCs) zilisema zinaidai serikali malimbikizo ya Sh34 bilioni lakini Wizara ya Petroli na Madini inashikilia kuwa kiasi cha pesa ambazo serikali inadaiwa na kampuni hizo ni Sh13 bilioni pekee.

Nayo Kampuni ya Usambazaji Mafuta Nchini (KPC) Jumamosi ilisema kuwa mafuta iliyoko katika hifadhi yake nchini inaweza kutosheleza mahitaji ya nchi hii kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo alisema kuwa kuna lita 69 milioni za mafuta aina ya Super Petrol, lita 94 milioni za dizeli, lita 13 milioni za mafuta taa na zaidi ya lita 23 milioni za mafuta ya ndege katika hifadhi zake kote nchini.

Serikali itoe pesa hizi haraka iwezekanavyo ili kuwaondolea Wakenya madhila yanayosababishwa na uhaba wa mafuta kama vile kupanda kwa nauli.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending