Connect with us

General News

Nina tajriba ya kufufua uchumi, Wanjigi asema – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Nina tajriba ya kufufua uchumi, Wanjigi asema – Taifa Leo

Nina tajriba ya kufufua uchumi, Wanjigi asema

NA KENYA NEWS AGENCY

MGOMBEA URAIS WA chama cha Safina, Jimmy Wanjigi amesema kuwa amehitimu vyema na ana tajriba ya kufufua uchumi wa nchi ndani ya muda mfupi.

Akizungumza Jumamosi akiwa Kaunti ya Murang’a, Wanjigi alisema nchi inategemea pesa za mikopo, akisema Kenya inahitaji rais atakayeokoa uchumi unaoporomoka.

Alisema hali ya sasa ya uchumi nchini inatokana na ufisadi mkubwa katika sekta ya umma ambayo imeacha Wakenya wengi wakiteseka kwa kushindwa kumudu bei za chakula na bidhaa za kimsingi.

Wanjigi alisisitiza kuwa atakuwa kwenye debe katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 akisema anaelewa kinachotatiza nchi na iwapo atamrithi Rais Uhuru Kenyatta, atafufua uchumi na kupunguza mateso ya mwananchi wa kawaida.

“Wale wanaoshindana nami kuwa rais wamekuwa katika siasa kwa miongo mingi na ninasema hawana kipya. Wakenya wakati huu wanahitaji kuchagua watu wapya ambao watamaliza ukosefu wa ajira, mfumko wa bei na kuleta maendeleo.”

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending