Connect with us

General News

Bei ya mafuta yavunja rekodi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Bei ya mafuta yavunja rekodi – Taifa Leo

Bei ya mafuta yavunja rekodi

Na JURGEN NAMBEKA

WAKENYA sasa watalazimika kulipa Sh9 zaidi kwa kila lita ya mafuta ya petroli, kulingana na ripoti ya ukaguzi wa bei iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EPRA).

Akizungumza katika makazi makuu ya mamlaka hiyo, mkurugenzi mkuu wa EPRA, Bw Daniel Kiptoo alieleza kuwa mafuta hayo yatauzwa kwa Sh144.62 kutoka Sh134.72.

Ongezeko hili ndilo la juu zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini. Kwa sasa mafuta aina ya Super Petrol yatauzwa kwa Sh145.03 mjini Eldoret, Sh144.14 Nakuru, Sh142.36 Mombasa, Sh144.62 Nairobi, Sh149.21 Lodwar, Sh146.55 Nanyuki na Sh145.03 Kisumu.

Kulingana na Bw Kiptoo mafuta yasiyosafishwa yaliongezeka bei, na kuchangia mabadiliko y bei ya mafuta kwenye pampu.

“Bei ya mafuta ambayo hayajasafishwa imeongezeka kutoka Sh7386 hadi Sh9832 kwa pipa. Ongezeko hili limechangia kupanda kwa bei ya mafuta,” alisema Bw Kiptoo.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa ongezeko la bei ya mafuta kwenye soko la dunia, lilisababisha mafuta ya petroli yauzwe kwa Sh173.70 kabla ya ruzuku ya serikali.

Kulingana naye, ukaguzi wa bei ulifanywa ili kusawazisha bei ya mafuta na kuwazuia Wakenya kutozwa zaidi na bei inavyopaswa.

Kulingana na Bw Kiptoo, Wakenya wanaotumia mafuta ya taa watalipia Sh113.44. Waendesha magari yanayotumia mafuta aina ya Diesel, watayalipia Sh125.50.

Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh111.19 jijini Mombasa, Sh113.44 Nairobi, Sh 113.29 Nakuru, Sh114.17 Eldoret, Sh118.35 Lodwar na Sh114.16 mjini Kisumu.

Ongezeko hilo la bei linajiri wakati ambao Wakenya wamekuwa wakishuhudia uhaba wa mafuta kote nchini, kwa takriban wiki tatu sasa.

Uhaba huu wa mafuta unakisiwa kuwa njama ya wauzaji wa mafuta kuficha mafuta, wakisubiri bei ya bidhaa hiyo muhimu ipande.

Akizungumza katika makao makuu ya wizara ya Kawi katika eneo la South C, Nairobi, Waziri wa Petroli na Uchimbaji wa Madini, Bi Monica Juma alieleza kuwa Kenya ina mafuta ya kutosha kwenye hifadhi yake hivyo uhaba huo ni njama tu.

“Ninaweza kuhakikisha kuwa tuna mafuta ya kutosha hapa nchini. Wauzaji kadhaa wa petroli wameenda kinyume na sheria ya nchi hii kwa kuficha mafuta wakisubiri ongezeko la bei. Tabia hii ni ya kibinafsi na inaenda kinyume na mamlaka waliyopewa wauzaji hawa,” alisema Bi Juma.

Alieleza kuwa serikali itamchukulia hatua yeyote atakayesababisha uhaba bandia, kwa manufaa yake binafsi.

“Muuzaji yeyote ambaye hayuko tayari kufuata sheria za nchi hii, ana uhuru wa kuondoka kwenye soko hili,” alisema Bi Juma.

Kulingana naye uhaba huu ambao umewahangaisha Wakenya unatarajiwa kusuluhishwa ndani ya saa 72 na kuwapa afueni Wakenya. Bi Juma aliwaomba Wauzaji kufanya kazi kwa saa 24 ili kuzuia misongamano ya magari, kwenye vituo vya kuuzia mafuta.

“Tumesikia taarifa za Wakenya kuamka saa sita za usiku kutafuta petroli, na inahuzunisha,” alisema Bi Juma.