Connect with us

General News

Jinsi miungano na vyama vya ushirika vinaweza kusaidia wakulima – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jinsi miungano na vyama vya ushirika vinaweza kusaidia wakulima – Taifa Leo

TUJIFUNZE UKULIMA: Jinsi miungano na vyama vya ushirika vinaweza kusaidia wakulima

NA SAMMY WAWERU

NIXON Mutai, Naibu Meneja kitengo cha Outgrowers katika kampuni ya James Finlay Kenya Ltd, anasema ikiwa kuna hatua ya busara waliyochukua baadhi ya wakulima wa majanichai Kericho na Bomet, ni kuwa kwenye miungano.

Chini ya makundi matano (primary cooperatives), yanayosimamiwa na Fintea Growers Cooperative Union, mahangaiko kupata soko yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Chama hicho cha ushirika, kwa ushirikiano na Finlays wana soko tayari la chai Uingereza, nchi za Uarabuni na Pakistani.

“Si bora soko, wanapata soko bora,” asema Mutai, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya majanichai.

Kutoka Kushoto: Afisa Mkuu Mtendaji wa Fintea Growers Cooperative Union, Nelson Ng’eno, Naibu Meneja Outgrowers-Finlays, Nixon Mutai na Meneja Outgrowers – Finlays, Geoffrey Chepkwony. PICHA | SAMMY WAWERU

Akiwa pia mkulima, anakumbuka changamoto alizopitia kutafutia mazao yake soko.

“Majanichai yanapokawia kupelekwa kiwandani baada ya kuchumwa huharibika upesi. Awali, kabla kuwa kwenye makundi, wakulima waliteseka, nao mabroka walitumia mwanya huo kuwakandamiza,” aelezea afisa huyo.

Kwa muda mrefu, wakulima wa majanichai nchini wamekuwa wakihangaika kupata soko bora.Kulingana na Mutai, mkondo ambao Fintea Growers imechukua ukiigwa na wakulima wote wa majanichai na mimea mingine, utawaletea afueni.

Mkulima Reuben Tanui kutoka Kericho anasema kabla mradi huo kuanzishwa, karibu akate tamaa kukuza majanichai.

“Ninahimiza wakulima wengine wawe kwenye miungano,” ashauri.

Kando na makundi hayo kupitia Fintea Growers na Finlays kuwatafutia soko lenye ushindani mkali, yanatumika kama jukwaa kuwahamasisha kulima mimea yenye thamani kama vile miparachichi na mseto wa mboga asilia.

“Pia, kuna wanaoendeleza ufugaji wa nyuki, kuku na ng’ombe wa maziwa kujipa pato la ziada badala ya kutegemea malipo ya chai pekee,” Mutai adokeza.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending