Connect with us

General News

Ripoti ya sakata ya sukari iliyotiwa sumu ya mercury ingali kitendawili – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ripoti ya sakata ya sukari iliyotiwa sumu ya mercury ingali kitendawili – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Ripoti ya sakata ya sukari iliyotiwa sumu ya mercury ingali kitendawili

MNAMO Novemba 21, 2018, Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Mamlaka na Hadhi ya Wabunge ilialika Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (EACC) kuchunguza madai ya wabunge kupokea hongo ili kuangusha ripoti kuhusu sakata ya uingizaji sukari bila kulipiwa ushuru.

Kamati hiyo chini ya Spika Justin Muturi, ilizitaka asasi hizo kuchunguza madai kuwa baadhi ya wabunge walihongwa kwa Sh10,000 chooni ili kuzima ripoti hiyo ya kamati ya bunge kuhusu sakata hiyo.

Lakini karibu miaka minne baadaye, asasi hizo zimeendelea kukimya kuhusu suala hilo licha ya kwamba, ripoti kuhusu sakata hiyo iliwaelekezea kidole cha lawama waliokuwa mawaziri Henry Rotich (Fedha) na Adan Mohamed (aliyekuwa Waziri wa Biashara ambaye sasa amejiuzulu kuwania ugavana wa Mandera).

EACC, DCI na Bunge la Kitaifa zisije zikasahau kuwa Wakenya bado wanataka wahusika katika sakata hiyo ya sukari iliyotiwa sumu ya mercury, na wabunge waliodaiwa kuhongwa, wachukuliwe hatua za kisheria.