[ad_1]
Alfred Keter kuhama UDA, kuwa mgombea huru Nandi Hills
NA FRED KIBOR
MBUNGE wa Nandi Hills, Alfred Keter amefichua kwamba atatetea kiti chake kama mgombea huru baada ya Kamati ya kutatua mizozo ya uteuzi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) kumpokonya cheti ikisema mchujo ulikumbwa na dosari nyingi.
Katika mahojiano na Taifa Leo, Bw Keter aliambia UDA wakutane kwenye debe katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na kutangaza kuwa atajiuzulu leo Jumatatu kutoka chama hicho kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto.
Kamati ya kutatua mizozo ya uteuzi ya UDA iliyojumuisha Collins Kiprono, Mary Mungai na Jadrian Kamotho Njenga ilisema kwamba Bw Bernard Kitur aliyepinga ushindi wa mbunge huyo alithibitisha kulikuwa na dosari kwenye mchujo wa kiti cha ubunge cha Nandi Hills.
Hata hivyo Bw Keter anasema uamuzi huo ulikuwa umepangwa ili kumpokonya cheti cha uteuzi.
“Kunyimwa cheti hakukuwa sadfa, ni njama iliyokuwa imepangwa. Sikuzua ghasia au kulazimisha nikabidhiwe cheti cha uteuzi ilivyosemwa katika kamati ya kutatua mizozo,” alisema.
“Nitajiuzulu kesho (leo Jumatatu) kutoka UDA na nitafanya kampeni kutetea kiti changu na ninajua nitashinda kwa kuwa nimefanyia maendeleo watu wa Nandi Hills,” alisema.
Next article
Mawaziri 54 kukutana Nairobi kujadili athari za corona kwa…
[ad_2]
Source link